Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

111 – Tunawapenda Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

112 – Hatuchupi mipaka katika kumpenda yeyote katika wao, wala hatujitengi mbali na yeyote katika wao.

113 – Tunawachukia wale wanaowachukia na kuwataja kwa njia isiyokuwa nzuri. Hatuwataji isipokuwa tu kwa njia nzuri.

114 – Kuwapenda ni dini, imani na wema.

115 – Kuwachukia ni ukafiri, unafiki na kuchupa mipaka.

MAELEZO

Hatuchupi mipaka katika kumpenda yeyote katika wao ambapo tukadai kuwa amekingwa na makosa, kama wanavosema Shiy´ah juu ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) na wengineo katika maimamu wao. Wala hatujitengi kutokana nao, kama walivofanya Raafidhwah. Wao wanaona kuwa haiwezekani kuwapenda watu wa nyumbani kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka kwanza mtu ajitenge mbali na Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Hata hivyo Ahl-us-Sunnah wanawapenda Maswahabah wote na wanawashusha ngazi zao wanazostahiki kwa uadilifu na inswafu, na si kwa matamanio na ushabiki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: l-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 101-102
  • Imechapishwa: 20/10/2024