Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

116 – Tunathibitisha ukhalifah baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wa kwanza ni Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhum), ambaye alifadhilishwa na kutangulizwa kabla ya ummah mzima, kisha ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh), kisha ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´ann) na kisha ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). Hawa ndio makhaliyfah waongofu na maimamu wenye kuongoza.

117 – Tunathibitisha Pepo juu ya wale kumi ambao walitajwa majina na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawaahidi Pepo. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni ya haki.

118 – Nao ni Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Twalhah, az-Zubayr, Sa´d, Sa´iyd, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah, ambaye ndiye mwaminifu wa Ummah huu. Allaah awawie radhi wote.

119 – Yule mwenye kuwazungumzia vizuri Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakeze waliosafishwa na kila najisi na kizazi chake waliotakaswa na kila uchafu, basi huyo amesalimika kutokana na unafiki.

120 – Wanazuoni wa Salaf katika wale waliotangulia na wa baada yao katika wale waliokuja baadaye ambao ni watu wema waliokuwa wanafata mapokezi na waliokuwa na ufahamu na uoni, haitakiw kuwataja isipokuwa kwa njia nzuri tu. Yule mwenye kuwataja kwa ubaya hafuati njia ya sawa.

MAELEZO

Kama alivosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

”Yeyote mwenye kutukana ukhaliyfah wa yeyote katika maimamu hawa basi ni mpotevu kuliko punda wa kufugwa.”[1]

[1] al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 116-117

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: l-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 20/10/2024