Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

108 – Allaah (Ta´ala) anaziitikia du´aa na kutatua mahitaji.

109 – Anakimiliki kila kitu na hakuna kitu kinachommiliki. Hakuna yeyote anayejitosheleza na Allaah (Ta´ala) kwa kiasi cha kupepesa jicho. Ambaye anaona kuwa anaweza kujitosheleza na Allaah kiasi cha kupepesa jicho, basi amekufuru na amekuwa miongoni mwa waliokula khasara.

110 – Allaah anaghadhibika na kuridhia, si kama yeyote katika viumbe.

MAELEZO

Hapa wanaraddiwa wakanushaji, wakiwemo Ashaa´irah, ambao wanakengeusha kughadhibika na kuridhika ni kutaka kufanya wema. Laiti ningelijua ni kwa nini wamekubali na kuamini kutaka na wakazikanusha sifa mbili zilizotajwa walizoamua kuzipindisha maana. Kama zilivyo sifa mbili hizo mja pia anasifiwa utashi. Ni kwa nini hawasemi juu ya sifa hizo mbili kama walivosema juu ya utashi wa kiungu, kwamba ni tofauti na utashi wa viumbe na unaolingana na yule msifiwa? Ibn Abiyl-´Izz (Rahimahu Allaah) amezungumzia hilo kwa undani, rejea huko.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 20/10/2024