68 – Abu Hurayrah ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Itapofika siku ya Qiyaamah Mola atawashukia waja.”
Ameipokea Muslim[1]. Hadiyth zinazozungumzia kushuka kwa Mola zimepokelewa kwa mapokezi tele. Nimetaja njia zake na kuzizungumzia kwa sababu nitakuja kuulizwa siku ya Qiyaamah – na hakuna kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah, Aliye juu kabisa, Mkubwa!
[1] Hili ni kosa. Muslim hakuipokea kabisa Hadiyth kwa tamko hili, isipokuwa ameipokea kwa cheni ya wapokezi aliyoitaja mtunzi wa kitabu katika ile ya asili. Kuhusiana na tamko hili, ameipokea at-Tirmidhiy (2/61), Ibn Khuzaymah (2/25 – muswada) na al-Haakim (1/418), kupitia njia nyingine kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye pia ameisahihisha.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 110
- Imechapishwa: 26/06/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)