Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia alimpiga mawe mwanamke anayetokana na Ghaamid baada ya kutubia na kumwomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amuadhibu. Wakati alipompuuza akamuuliza kama anataka kumrudisha nyuma kama alivyomrudisha nyuma Maa´iz. Anamuomba amuadhibu kwa king´ang´anizi baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwamrisha aende kumnyonyesha mtoto wake kwa muda wa miaka miwili. Baada ya miaka miwili mwanamke huyo akarudi tena kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mara ya pili, akiwa pamoja na mtoto wake akila mkate ili kumuonyesha kuwa hamuhitaji tena mama yake. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha zifungwe vizuri nguo zake, achimbiwe shimo na kupigwa mawe. Baada ya hapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamswalia swalah ya jeneza, jambo linalojulisha kuwa ni miongoni mwa watu wa Peponi. Kwa sababu mtubiaji amerehemewa na mwenye kurehemewa Allaah (´Azza wa Jall) anamwingiza Peponi. ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alisema: “Ee Mtume wa Allaah! Unamswalia baada ya yeye kuzini?” Akasema: “Akasema: “Hakika ametubia tawbah ambayo iwapo itagawanywa kwa watu sabini wa Madiynah basi ingeliwaenea. Je, kuna tawbah bora kushinda kwamba amejileta mwenyewe kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall)?”
Haya ndio yanayothibitishwa na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na daima wanaifanyia kazi hukumu na ´Aqiydah hii.
Kuna uwezekano wa kuadhibiwa juu ya uzinzi hata kama mtu hakukiri dhambi yake. Wanaume wawili waadilifu wakishuhudia kuwa amezini, anaadhibiwa ingawa hakukiri mwenyewe. Ushahidi wao unatakiwa kufanana na wasitofautiane ya kwamba wamemuona kikweli mzinifu wa kiume akimzini mzinifu wa kike. Baada ya hapo watenda madhambi hao wataadhibiwa, ima kwa kupigwa bakora au kwa kupigwa mawe.
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 148-149
- Imechapishwa: 23/06/2026
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia alimpiga mawe mwanamke anayetokana na Ghaamid baada ya kutubia na kumwomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amuadhibu. Wakati alipompuuza akamuuliza kama anataka kumrudisha nyuma kama alivyomrudisha nyuma Maa´iz. Anamuomba amuadhibu kwa king´ang´anizi baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwamrisha aende kumnyonyesha mtoto wake kwa muda wa miaka miwili. Baada ya miaka miwili mwanamke huyo akarudi tena kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mara ya pili, akiwa pamoja na mtoto wake akila mkate ili kumuonyesha kuwa hamuhitaji tena mama yake. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha zifungwe vizuri nguo zake, achimbiwe shimo na kupigwa mawe. Baada ya hapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamswalia swalah ya jeneza, jambo linalojulisha kuwa ni miongoni mwa watu wa Peponi. Kwa sababu mtubiaji amerehemewa na mwenye kurehemewa Allaah (´Azza wa Jall) anamwingiza Peponi. ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alisema: “Ee Mtume wa Allaah! Unamswalia baada ya yeye kuzini?” Akasema: “Akasema: “Hakika ametubia tawbah ambayo iwapo itagawanywa kwa watu sabini wa Madiynah basi ingeliwaenea. Je, kuna tawbah bora kushinda kwamba amejileta mwenyewe kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall)?”
Haya ndio yanayothibitishwa na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na daima wanaifanyia kazi hukumu na ´Aqiydah hii.
Kuna uwezekano wa kuadhibiwa juu ya uzinzi hata kama mtu hakukiri dhambi yake. Wanaume wawili waadilifu wakishuhudia kuwa amezini, anaadhibiwa ingawa hakukiri mwenyewe. Ushahidi wao unatakiwa kufanana na wasitofautiane ya kwamba wamemuona kikweli mzinifu wa kiume akimzini mzinifu wa kike. Baada ya hapo watenda madhambi hao wataadhibiwa, ima kwa kupigwa bakora au kwa kupigwa mawe.
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 148-149
Imechapishwa: 23/06/2026
https://firqatunnajia.com/66-mtubiaji-ni-mwenye-kusamehewa/