65. Mamlaka pekee ndio yanayotekeleza adhabu

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

Kumpiga mawe mzinifu aliyeoa/kuolewa au aliwahi kuoa/kuolewa ni haki endapo atakiri mwenyewe au kukawepo ushahidi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipiga mawe na wale viongozi waongofu pia walipiga mawe.

MAELEZO

Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah inapokuja katika kumsimamishia adhabu mzinzi ambaye kishawahi kuingia katika ndoa. Anatakiwa kutekelezewa Shari´ah ya Allaah takasifu na hukumu Zake zilizoshinda. Mtu kama huyo anapaswa kupigwa mawe hadi afariki baada ya kuhukumiwa hivo na yule hakimu wa Kishari´ah ambaye kateuliwa na mtawala wa waislamu. Mkusudiwa ni yule mtu ambaye amewahi kuingia ndani ya ndoa sahihi; huyu ndiye ambaye atapigwa mawe hadharani hadi kufa. Kuna matarajio Allaah akamsamehe dhambi yake na kumwingiza Peponi.

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 146
  • Imechapishwa: 23/06/2026