Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

وَإِذَا غَشِيَهُم مَّوْجٌ كَالظُّلَلِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

“Na yanapowafunika mawimbi kama vivuli humwomba Allaah wakimtakasia dini Yake.” (31:32)

MAELEZO

Hii pia ni kama zile Aayah mbili zilizotangulia ambayo inafahamisha namna washirikina hawa walikuwa wakishirikisha tu wakati wa raha. Inapofika wakati wa shida, wanamwelekea Allaah peke Yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 77
  • Imechapishwa: 25/11/2023