Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Ikiwa nguzo hata moja itaachwa, sawa kwa kukusudia, au kutokukusudia swalah inabatilika kwa kuiacha.
Ikiwa jambo la wajibu litaachwa kwa kukusudia, swalah yabatilika kwa kuliacha, na ikiwa litaachwa kwa kutokukusudia, itakuwa ni wajibu kuleta Sujuud ya kusahau.
MAELEZO
Nguzo za swalah, mambo yake ya wajibu na mambo yake yanayopendeza vyote ni sehemu ya swalah na vinaingia katika maana ya Kisharia ya swalah, ambayo ni:
“Maneno na matendo maalum yanayoanzwa kwa Takbiyr na kuhitimishwa kwa salamu.”
Kuna tofauti kati ya nguzo, wajibu na mambo yanayopendeza:
1 – Nguzo ni lazima kuzifanya na wala haziwezi kusamehewa ikiwa mtu ataziacha, ni mamoja ameaziacha kwa kusahau au kwa makusudi.
2 – Mambo ya wajibu kuyaacha kwa makusudi kunabatilisha swalah. Hata hivyo kuziacha kwa kusahau kunaweza kusahihishwa kwa Sujuud ya kusahau.
3 – Mambo yanayopendeza, kama vile du´aa ya kufungulia swalah na kuomba kinga, ni kwamba anayeyatekeleza hupata thawabu na anayeyaacha haadhibiwi isipokuwa iwapo kuacha kwake kunatokana na kuachana na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Basi yule mwenye kuiacha Sunnah yangu si katika mimi.”
Ameipokea al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1401).
Hakika neno Sunnah katika Hadiyth hii lina maana pana zaidi ya matumizi mengine ya neno hilo. Maana yake ni njia yake na yote aliyokuwa akiyafanya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hilo linajumuisha kila kilichokuja katika Kitabu cha Allaah na Sunnah zake Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Hiki ndicho kilichowezekana kufasiri katika maelezo ya sharti za swalah, nguzo zake na mambo yake ya wajibu cha Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Ninamuomba Allaah (´Azza wa Jall) amsamehe, amuongezee thawabu na malipo kwa juhudi zake kubwa katika kunusuru dini na kuhimiza kushikamana na Qur-aan, Sunnah, na mfumo wa Salaf. Ninamuomba Yeye (Ta´ala) awape waislamu uelewa katika dini na uthabiti juu ya haki. Kwani hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kujibu maombi.
Swalah, salamu na baraka zimwendee mja na Mtume wake Muhammad, jamaa zake na Maswahabah zake wote.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 93-94
- Imechapishwa: 06/07/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 93-94
Imechapishwa: 06/07/2026
https://firqatunnajia.com/65-tofauti-kati-ya-sharti-nguzo-na-mambo-ya-wajibu-ya-swalah/