Shaykh (Rahimahu Allaah) amesema kwamba imamu na anayeswali peke yake wanatakiwa kusema:

سمع الله لمن حمده

”Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”,

na si maamuma, jambo ambalo ndio sahihi. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika imamu amewekwa ili afuatwe… ” na ndani yake imekuja: “Anaposema:

سمع الله لمن حمده

”Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”,

semeni:

ربنا ولك الحمد

”Mola wetu, himdi zote ni Zako.”

Ameipokea al-Bukhaariy (732–734) kupitia kwa Anas na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhumaa). Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth hizo mbili: ”Semeni:

ربنا ولك الحمد

”Mola wetu, himdi zote ni Zako.”

Hakusema: ”Semeni:

سمع الله لمن حمده

”Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

Baadhi ya wanazuoni wameona kuwa maamuma pia anatakiwa kusema:

سمع الله لمن حمده

”Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

hali ya kujengea hoja ujumla wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya Maalik bin al-Huwayrith:

“Swalini kama mnavyoniona ninaswali.”

Ameipokea al-Bukhaariy (631).

Njia ya hoja ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

سمع الله لمن حمده

”Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

Kwa hivyo mamuma pia wanatakiwa kusema:

سمع الله لمن حمده

”Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

Kuhusu Hadiyth inayosema: “Anaposema:

سمع الله لمن حمده

”Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”,

semeni:

ربنا ولك الحمد

”Mola wetu, himdi zote ni Zako.”

ni yenye kufungamanishwa na Hadiyth isemayo:

“Swalini kama mnavyoniona ninaswali.”

Hilo ni kama mfano wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mnaposikia adhaana basi semeni kama anavyosema muadhini.”

Ameipokea al-Bukhaariy (611) na Muslim (383) kupitia kwa Abu Sa’iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ‘anh). Hadiyth hiyo imefungamanishwa na Hadiyth isemayo:

حي على الصلاة، حي على الفلاح

”Njooni katika swalah, njooni katika mafanikio.”

Mwitikiaji anatakiwa kusema:

لا حول ولا قوّة إلاّ بالله

”Hapana kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

Hivo ndivo imekuja katika ”as-Swahiyh” ya Muslim (385) kupitia kwa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anh).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 91-93
  • Imechapishwa: 06/07/2026