Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

وَوَيْلٌ لِّلْمُشْرِكِينَ الَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ

“Na ole kwa washirikina. Ambao hawatoi zakaah nao ni wenye kuikanusha Aakhirah.”[1]

Nini makusudio yake?

Jibu: Inaweza kuwa na maana mbili:

1 – Makusudio ya zakaah ni utakaso wa nafsi, kwa maana ya kuisafisha kutokana na shirki. Amesema (Ta´ala) amesema:

قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا

“Hakika amefaulu yule aliyeitakasa.”[2]

Kutokana na tafsiri hiyo Aayah inawakusudia washirikina wasiojitakasa kutokana na shirki na njia zake.

2 – Zakaah ya aina ya kujitolea mali. Kwa hiyo kule kujizuia kwao kutoa zakaah inakuwa ni moja katika sifa zao. Ingawa watatoa zakaah au wakafanya aina nyingine ya ´ibaadah basi yasingekubaliwa kutoka kwao kutokamana na shirki yao.

[1] 41:6-7

[2] 91:9

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/15-16)
  • Imechapishwa: 05/07/2026