Swali: Je, inafaa kwa cherehani kuwashonea wanaume nguo zinazoshuka chini ya vifundo vya miguu?
Jibu: Hapana. Kuvaa nguo inayoshuka chini ya kongo za miguu ni dhambi kubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kile kikoi kilicho chini ya mafundo mawili ya miguu kiko ndani ya Moto.”[1]
Haya ni makemeo na matahadharisho makali. Kila dhambi iliyotajwa sambamba na makemeo ni katika madhambi makubwa. Yule anayewashonea wanaume nguo inayovuka vifundo vya miguu ameshirikiana nao katika dhambi hii kubwa naye amepata fungu lake. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ
“Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah; hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (5787).
[2] 05:02
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/310-311)
- Imechapishwa: 05/07/2026
Swali: Je, inafaa kwa cherehani kuwashonea wanaume nguo zinazoshuka chini ya vifundo vya miguu?
Jibu: Hapana. Kuvaa nguo inayoshuka chini ya kongo za miguu ni dhambi kubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kile kikoi kilicho chini ya mafundo mawili ya miguu kiko ndani ya Moto.”[1]
Haya ni makemeo na matahadharisho makali. Kila dhambi iliyotajwa sambamba na makemeo ni katika madhambi makubwa. Yule anayewashonea wanaume nguo inayovuka vifundo vya miguu ameshirikiana nao katika dhambi hii kubwa naye amepata fungu lake. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ
“Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah; hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (5787).
[2] 05:02
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/310-311)
Imechapishwa: 05/07/2026
https://firqatunnajia.com/cherehani-anawashonea-wanaume-nguo-inayovuka-vifundo-vya-miguu/