Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Ya wajibu ni mambo nane:
1 – Takbiyr zote mbali na Takbiyrat-ul-Ihraam.
2 – Kusema:
سبحان ربي العظيم
“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”
katika Rukuu´.
3 – Kusema:
سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَه
“Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”
kwa imamu na kwa anayeswali peke yake.
4 – Kusema:
رَبَّنَا وَ لَكَ الْحَمْدُ
”Ee Mola Wetu! Ni Zako himdi zote.”
Itasemwa na wote.
5 – Kusema:
سبحان ربي الأعلى
“Ametakasika Mola wangu Aliye juu kabisa.”
katika Sujuud.
6 – Kusema:
رَبِّ اغْفِرْ لِي
“Mola! Nisamehe!”
baina ya Sujuud mbili.
7 – Tashahhud ya kwanza.
8 – Kukaa katika Tashahhud hiyo.
MAELEZO
Mambo yote haya ya wajibu ni ya kimatamshi isipokuwa tu moja katika mambo hayo ambayo ni ya kivitendo; kukaa katika Tashahhud ya kwanza. Ibn Qudaamah amesema katika kitabu chake ”al-Mughniy” (2/180) ya kwamba uwajibu wa mambo haya saba ya kimaneno ndio jambo linalotambulika kwa Ahmad na kwamba maoni yanayosema kuwa sio wajibu ndio ya wanazuoni wengi. Amesema:
”Kinachotambulika kutoka kwa Ahmad ni kuleta Takbiyr wakati wa kushuka na kuinuka, Tasbiyh katika Rukuu´ na Sujuud, kusema:
سمع الله لمن حمده
”Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”,
kusema:
ربنا ولك الحمد
”Mola wetu, himdi zote ni Zako.”,
kusema:
ربي اغفر لي
”Mola wangu, nisamehe.”
baina ya sijda mbili na Tashahhud ya kwanza ni mambo ya wajibu. Haya pia ndio maoni ya Ishaaq na Daawuud. Pia kuna riwaya kutoka kwa Ahmad kuwa si wajibu, ambayo ndiyo maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni.”
Miongoni mwa mambo ambayo Ibn Qudaamah ameyatumia kama dalili katika ”al-Mughniy” ni maneno yake:
”Abu Daawuud amepokea kutoka kwa ´Aliy bin Yahyaa bin Khallaad kutoka kwa ami yake, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:
”Haitimii swalah ya mtu yeyote mpaka atawadhe… ” mpaka aliposema: ”… kisha alete Takbiyr, kisha arukuu mpaka viungo vyake vipate utulivu, kisha aseme:
سمع الله لمن حمده
”Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”
mpaka asimame wima, kisha aseme:
الله أكبر
”Allaah ni Mkubwa.”
kisha asujudu mpaka awe ametulia kwenye Sujuud, kisha aseme:
الله أكبر
”Allaah ni Mkubwa.”
na anyanyue kichwa chake mpaka akae sawa, kisha aseme:
الله أكبر
”Allaah ni Mkubwa.”
kisha asujudu mpaka viungo vyake vitulie, kisha anyanyue kichwa chake na alete Takbiyr. Akifanya hivyo basi swalah yake imekamilika.”
Hii ni dalili juu ya ulazima wa kuleta Takbiyr. Hadiyth iko katika ”Sunan Abiy Daawuud” (857) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 89-91
- Imechapishwa: 05/07/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 89-91
Imechapishwa: 05/07/2026
https://firqatunnajia.com/63-mambo-ya-wajibu-ya-ndani-ya-swalah/