65. Dalili kwamba watu wa kale walikuwa wakishirikisha katika kipindi cha raha peke yake

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّـهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ

“Je mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah au ikakufikieni Qiyaamah; je, mtamwomba asiyekuwa Allaah mkiwa ni wakweli?” Bali Yeye pekee ndiye mtayemwomba kisha atakuondoleeni yale mliyomwomba akitaka na mtasahau mnayoyashirikisha.” (06:40-41)

وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ ضُرٌّ دَعَا رَبَّهُ مُنِيبًا إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا خَوَّلَهُ نِعْمَةً مِّنْهُ نَسِيَ مَا كَانَ يَدْعُو إِلَيْهِ مِن قَبْلُ وَجَعَلَ لِلَّـهِ أَندَادًا لِّيُضِلَّ عَن سَبِيلِهِ ۚ قُلْ تَمَتَّعْ بِكُفْرِكَ قَلِيلًا ۖ إِنَّكَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ

“Na inapomgusa mtu dhara, basi humwomba Mola wake akirudiarudia kutubia Kwake, kisha Akimruzuku neema kutoka Kwake husahau yale aliyokuwa akimwomba kabla na kumfanyia Allaah wenza ili apotoke kutokamana na njia Yake. Sema: “Starehe kwa kufuru yako kidogo tu – hakika wewe ni miongoni mwa watu wa Motoni.”” (39:08)

MAELEZO

Aayah hizi zinafahamisha kuwa walikuwa wakimshirikisha Allaah wakati wa shida tu. Wanapofikwa na adhabu au Qiyaamah, hawamuabudu mwengine asiyekuwa Allaah. Amesema (Ta´ala):

بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ

“Bali Yeye pekee ndiye mtayemwomba kisha atakuondoleeni yale mliyomwomba akitaka na mtasahau mnayoyashirikisha.”

Katika hali hii wanasahau waungu wao na hawamuombi mwengine asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall).

Mtu anapofikwa na tatizo, basi anamuomba Allaah kwa kumlilia. Lakini akimpa neema kutoka Kwake husahau yale aliyokuwa akimwitia zamani na akamfanyia Allaah washirika ili apoteze watu njia Yake. Anashirikisha katika kipindi cha raha wakati anatakasa dini wakati wa shida.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 77
  • Imechapishwa: 25/11/2023