65. Athar ”Wakati kulipoteremshwa… ”

65 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: as-Sarriy bin Yahyaa ametuhadithia: Nimemsikia al-Hasan akisema:

”Wakati kulipoteremshwa:

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Mtume. Hivyo enyi walioamini mswalieni na mumsalimu kwa salamu.”[1]

wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Tumejua namna ya kukutakia amani; unatuamuru vipi kukuswalia?” Akasema: ”Semeni: ”Ee Allaah! Weka sifa Zako na baraka Zako kwa jamaa zake Muhammad kama Ulivyoziweka kwa jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Allaah amewatuma kama alivyonituma mimi.”[2]

[1] 33:56

[2] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh lakini kuna Swahabah anayekosekana. al-Hasan huyu ni al-Hasan bin Abiyl-Hasan al-Baswriy. Ibn Abiy Shaybah ameipokea kupitia njia nyingine kutoka kwake pasi na kutaja Aayah.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 62-63
  • Imechapishwa: 29/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy