64. Athar “Tumejua namna ya kukutakia amani… ”

64 – Mahmuud bin Khidaash ametuhadithia: Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Abu Ma´shar, kutoka kwa Ibraahiym, ambaye amesimulia:

”Walisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Tumejua namna ya kukutakia amani, ni namna gani ya kukuswalia?” Akasema: ”Semeni:

اللهم صل على عبدك و رسولك و أهل بيته، كما صليت على آل إبراهيم، إنك حميد مجيد. و بارك عليه و أهل بيته، كما باركت على إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu mja na Mtume Wako na watu wa familia yake kama Ulivyowasifu jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa. Na mbariki yeye na watu wa familia yake kama Ulivyombariki Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh lakini kuna Swahabah anayekosekana. Ibraahiym huyu ni Ibn Yaziyd an-Nakha´iy. Amesimulia kutoka kwa wanafunzi wakubwa wa Maswahabah, akiwemo Masruuq, al-Aswad, ´Abdur-Rahmaan bin Yaziyd na ´Alqamah. AbU Ma´shar jina lake ni Ziyaad bin Kulayb. al-Mughiyrah ni Ibn Miqsam adh-Dhwabbiy na Jariyr ni Ibn ´Abdil-Hamiyd.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 62
  • Imechapishwa: 29/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy