66. Hadiyth “Tumejua namna ya kukutakia amani… ”

66 – Ishaaq al-Farwiy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ja´far ametuhadithia, kutoka kwa Ibn-ul-Haad, kutoka kwa ´Abdullaah bin Khabbaab, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy, ambaye amesema:

”Ee Mtume wa Allaah! Tumejua namna ya kukutakia amani, ni namna gani ya kukuswalia?” Akasema: ”Semeni:

اللهم صل على محمد عبدك و رسولك، كما صليت على آل إبراهيم، و بارك علىى محمد و على آل محمد، كما باركت على إبراهيم

”Ee Allaah! Msifu Muhammad, mja na Mtume wako, kama Ulivyowasifu jamaa zake Ibraahiym. Na mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym.”[1]

[1] Hadiyth Swahiyh. Mbali na ´Abdullaah bin Ja´far, ambaye alikuwa baba yake ´Aliy al-Madiyniy, wanamme wake wote ni waaminifu. Kama tulivosema alikuwa dhaifu. Hata hivyo hakuisimulia peke yake. Wameipokea wengine kadhaa akiwemo al-Bukhaariy, an-Nasaa´iy na al-Bayhaqiy kupitia njia nyingine kutoka kwa Ibn-ul-Haad. Vivyo hivyo ndivo amefanya mtunzi katika Hadiyth inayofuatia. Ibn-ul-Haad jina lake ni Yaziyd bin ´Abdillaah bin al-Haad.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 63-64
  • Imechapishwa: 29/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy