64. Ni kina nani walikuwa wajumbe wa mwaka wa 9?

Swali 64: Ni kina nani walikuwa wajumbe wa mwaka huu waliofuatana katika mpangilio wa matukio?

Jibu: Ujumbe wa Tamiym. Kuhusiana na hilo kukateremshwa:

إِنَّ الَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَاءِ الْحُجُرَاتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ

”Hakika wale wanaokuwita nyuma ya vyumba wengi wao hawatii akilini.”[1]

Ujumbe wa ´Abdul-Qays. Walifika kabla ya Ufunguzi.

Ujumbe wa Banuu Haniyfah. Miongoni mwao alikuwepo Musaylimah Mwongo.

Ujumbe wa Najraan. Kuliteremshwa juu yao zile Aayah 83 za mwanzo wa Suurah ”Aal ´Imraan”.

Ujumbe wa Banuu ´Aamir.

Ujumbe wa Dhwimaam bin Tha´labah.

Ujumbe wa Tway´ pamoja na Zayd bin al-Khayl.

Ujumbe wa ´Adiy bin Haatim.

Ujumbe wa Daws huko Khaybar. Uliongozwa na at-Twufayl. Alifika kabla ya Ufunguzi na akaingia katika Uislamu.

Ujumbe wa Ash´ariyyuun pamoja na wale Wahajiri waliofanya Hijrah mara mbili.

Ujumbe wa Farwah bin Musayk al-Muraadiy kwa niaba ya watu wake.

Ujumbe wa Azd.

Ujumbe wa al-Ash´ath bin Qays al-Kindiy.

Mjumbe wa wafalme wa Himyar ambaye alitangaza Uislamu wa watu wake pamoja na barua ya Dhuu Yazan. Kwa hiyo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliwarudishia barua inayotambulika sana ya ´Amr bin Hazm.

Ujumbe wa Jariyr al-Bajaliy.

Ujumbe wa Waa-il bin Hujr.

Ujumbe wa Abu Raziyn al-´Uqayliy.

Ujumbe wa Sudaa´.

Ujumbe wa al-Haarith al-Bakriy.

Ujumbe wa Ashjaa´.

Ujumbe wa Farwah al-Judhaamiy. Warumi wakamuua.

Ujumbe wa Tamiym bin Aws ad-Daariy.

Ujumbe wa Fizaarah.

Ujumbe wa Asad.

Ujumbe wa Banuu ´Abs. Ulikuwa kabla ya Ufunguzi na kabla ya mkataba wa Hudaybiyah.

Ujumbe wa Banuu Murrah.

Ujumbe wa Banuu Tha´labah huko Ji´irraanah.

Ujumbe wa Banuul-Haarith katika mwaka wa 10 wakati wa hijjah ya kuaga.

Ujumbe wa Banuu Kilaab.

Ujumbe wa Banuu ´Aqiyl Ka´b.

Ujumbe wa Banuu Qushayr bin Ka´b.

Ujumbe wa Kinaanah.

Ujumbe wa Baahilah.

Ujumbe wa Banuu Sulaym kabla ya Ufunguzi ambao walioushuhudia.

Ujumbe wa Hilaal bin ´Aamir.

Ujumbe wa Banuu Bakr.

Ujumbe wa Taghlab.

Ujumbe wa Tujiyb kutokea Yemen.

Ujumbe wa Khawlah mwaka wa 10.

Ujumbe wa Ju´fiy.

Ujumbe wa Azd.

Ujumbe wa Banuu Sa´d Hudhaym.

Ujumbe wa Bahraa´.

Ujumbe wa Udhrah.

Ujumbe wa Baliy. Miongoni mwao walikuwepo waulizaji kuhusu kilichookotwa.

Ujumbe wa Ghassaan mwaka wa 10.

Ujumbe wa Ghaamid mwaka wa 10.

Ujumbe wa Nakha´iy. Huu ndio ulikuwa ujumbe wa mwisho na ulitokea Muharram mwaka wa 11.

[1] 49:04

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 126-131
  • Imechapishwa: 30/10/2023