Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
102 – Matendo ya viumbe yameumbwa na Allaah na ni machumo ya waja.
103 – Allaah (Ta´ala) hakuwalazimisha kufanya isipokuwa yale wanayoyaweza, na wala hawawezi kufanya isipokuwa yale aliyowalazimisha. Hiyo ndio tafsiri ya hapana kutikisika wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Hakuna yeyote awezaye kumuasi Allaah isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Wala hakuna yeyote awezaye kumtii Allaah kwa kudumu isipokuwa kwa kuwafikishwa na Allaah (Ta´ala).
MAELEZO
Bi maana hawawezi isipokuwa yale ambayo Allaah amewawezesha. Uwezo huo ndio kunamaanishwa kuwafikishwa, na si uzima, uwezo na usalama. Lakini kuna tatizo katika maneno ya mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah), jambo ambalo amelibainisha Ibn Abiyl-´Izz na akasema:
”Kukalifishwa hakutumiwi kwa maana ya kuweza, isipokuwa kunatumiwa kwa maana ya amri na makatazo. Hapa amesema ”hakuwalazimisha kufanya isipokuwa yale wanayoyaweza na wala hawawezi kufanya isipokuwa yale aliyowalazimisha”. Udhahiri wake ni kwamba yanarejea katika maana moja, jambo ambalo si sahihi. Kwa sababu wanaweza zaidi ya yale waliyolazimishwa, lakini Anachotaka (Subhaanah) kwa waja Wake ni kuwarahisishia na kuwawepesishia:
يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ
”Allaah anakutakieni mepesi na wala hakutakieni magumu.”[1]
يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا
“Allaah anataka kukukhafifishieni, kwani mtu ameumbwa dhaifu.”[2]
وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ
“Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika dini.”[3]
Lau tungelazimishwa zaidi ya yale tuliyowajibishiwa, tungeliyaweza. Lakini ametutunuku, ameturehemu na ameturahisishia na hakutujaalia katika dini yetu mambo yoyote mazito. Jawabu la tatizo hili ni katika yale yaliyokwishatangulia: ya kwamba uwezo uliokusudiwa ni upande wa kuwafikishwa, na si uwezo na usalama. Kuna utatizi katika matamshi, hivyo lizingatie hilo.”[4]
[1] 2:185
[2] 4:28
[3] 22:78
[4] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 655-656
- Muhusika: Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 95-96
- Imechapishwa: 16/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)