64. Adabu ya nne iliyopendekezwa: Kumshukuru Allaah kwa neema ya kufunga

Miongoni mwa adabu za funga ni mfungaji ahudhurishe hadhi ya neema ya Allaah juu yake kwa kufunga kwa vile amemuwafikisha na akamfanyia wepesi mpaka akatimiza siku yake na akakamilisha mwezi wake. Watu wengi hunyimwa kufunga ima kwa kufariki kwao kabla ya yenyewe kufika, kushindwa kwao, upotofu wao na kuipuuza kwao kuitekeleza. Hivyo mfungaji amshukuru Mola Wake juu ya neema ya funga ambayo ni sababu ya kusamehewa kwa madhambi, kufuta makosa na kupandishwa daraja katika Nyumba ya neema tele jirani ya Mola mkarimu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 79
  • Imechapishwa: 27/04/2021