27. Mtumzima kikongwe na mgonjwa aliye na maradhi sugu katika Ramadhaan

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewawajibishia waislamu kufunga kwa hali ya kutekeleza kwa wale wasiokuwa na udhuru na kwa hali ya kulipa kwa wale wenye udhuru ambao wanaweza kulipa katika masiku mengine. Kuna sampuli nyingine ya tatu ambao hawawezi kwa hali ya kutekeleza wala kulipa. Mfano wa watu hawa ni kama mzee kikongwe na mgonjwa ambaye hakutarajiwi kupona kwake. Aina hii Allaah amewawepesishia. Badala ya kufunga Allaah amewawajibishia kumlisha masikini chakula kwa kila siku moja. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

”Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ

”Kwa wale wanaoiweza lakini kwa tabu watoe fidia kumlisha masikini.”[2]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Hiyo ni kuhusu mtumzima ambaye hawezi kufunga.”

Ameipokea al-Bukhaariy[3].

Mgonjwa mwenye maradhi yasiyotarajiwa kupona ana hukumu moja kama mzee. Hivyo atamlisha masikini kwa kila siku moja.

[1] 02:286

[2] 02:184

[3] (4505).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/390-391)
  • Imechapishwa: 27/04/2021