2 – ´Aaishah ameeleza kuhusiana na Kisa cha Usingiziaji:

”Wakati nilipokuwa nimekaaa kambini kwangu nilichukuliwa na usingizi. Swafwaan bin al-Mu´twil as-Sulamiy adh-Dhakwaaniy alikuwa akiondoka nyuma ya jeshi na akisafiri mapema usiku. Asubuhi akafika kwenye kambi yangu na akaona mtu amelala. Akanisogelea na akanitambua wakati aliponiona kwa sababu alikuwa amekwishaniona kabla ya kufaradhishwa hijaab. Nikaamshwa wakati aliposema: ”Hakika sisi ni wa Allaah na Kwake ndio tutarejea” wakati aliponijua. Ndipo nikajifunika uso wangu kwa jilbaab yangu… ”[1]

[1] al-Bukhaariy (8/365-388) pamoja na Fath-ul-Baariy, Muslim (8/113-118), Ahmad (6/194-197), Ibn Jariyr (18/62-66) na Abul-Qaasim al-Hanaa’iy katika ”al-Fawaa-id” (9/142/2) ambaye amesema kuwa ni nzuri. Upokezi mwingine na ziada ni kutoka kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 106
  • Imechapishwa: 03/10/2023