61. Mshirikina anashuhudia dhidi ya nafsi yake mwenyewe

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Akisema: “Ni yule mwenye kuuelekea mti, jiwe au nyumba iliyojengwa kwenye kaburi n.k., anawaomba, anawachinjia na kusema: “Vinatukurubisha kwa Allaah na Allaah anatulinda [na madhara] kwa baraka zake na anatupa baraka Zake” Mwambie: “Umesema kweli. Na haya ndio yaleyale mnayoyafanya kwenye mawe, manyumba yaliyo kwenye makaburi na mengineyo.” Hili amelikubali ya kwamba kitendo chao hichi ni kuabudu masanamu, na hili ndilo lililokuwa linatakikana.

MAELEZO

Hiki ni kinyume cha maneno yetu “Hili ni dai linalokadhibishwa na Qur-aan”. Akisema shirki ni kuuelekea mti, jiwe au nyumba iliyojengwa kwenye kaburi n.k., anawaomba, anawachinjia na kusema kwamba vinawakurubisha kwa Allaah, tunamwambia: “Umesema kweli. Haya ndio yaleyale unayoyafanya. Kwa hivyo unakuwa mshirikina kwa kushuhudia dhidi ya nafsi yako mwenyewe – na hili ndilo lilolokuwa likitarajiwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 73
  • Imechapishwa: 25/11/2023