Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Akisema: “Shirki ni kuabudu masanamu, na sisi hatuabudu masanamu” Mwambie: “Na nini maana ya kuabudu masanamu? Unafikiria ya kwamba walikuwa wanaamini kuwa miti ile na mawe yale yanaumba, yanaruzuku na yanaendesha mambo kwa yule anayeviomba? Hili ni dai linalokadhibishwa na Qur-aan!”

MAELEZO

Mshirikina akisema kuwa shirki maana yake ni kuabudia masanamu, na wao hawayaabudii masanamu, ataulizwa maswali mawili:

1 – Nini maana ya kuabudia masanamu? Unafikiri kuwa waliokuwa wakiyaabudu walikuwa wakiamini kuwa yanaumba, yanaruzuku na yanamuendeshea mambo yule anayeyaomba? Haya ni madai yanayokadhibishwa na Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 73
  • Imechapishwa: 25/11/2023