Maneno yake:
”… na kupangilia kati ya kila nguzo.”
Nguzo ya kumi miongoni mwa nguzo za swalah ni kupangilia kati ya kila nguzo. Ni lazima zipangiliwe. Mtu aanze kuleta Takbiyrat-ul-Ihraam, kisha asome al-Faatihah na kisha arukuu. Iwapo ataleta Takbiyrat-ul-Ihraam, kisha akarukuu, kisha akasoma al-Faatihah au akasujudu halafu akasimama na kurukuu hakupangilia. Kwa hiyo swalah yake inabatilika.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 90
- Imechapishwa: 24/06/2022