Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ni lazima kuwa na utulivu katika vitendo vyote na kupangilia kati ya kila nguzo. Dalili ni Hadiyth kutoka kwa Abu Hurayrah kuhusiana na mtu aliyekuwa akiswali vibaya. Kasema:

“Wakati tulipokuwa tumekaa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuliingia mtu, akaswali kisha akamsalimia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akamwambia “Rudi ukaswali, hakika hujaswali.” Alifanya hivi mara tatu. Mwishoni akamwambia: “Naapa kwa yule aliyekutuma kwa haki; siwezi bora zaidi ya hivi. Nifunze!” Akasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Unaposimama kutaka kuswali, lete Takbiyr. Kisha soma uwezacho katika Qur-aan. Kisha utarukuu mpaka unyooke. Kisha utasimama sawa sawa. Kisha utasujudu mpaka utapotulia katika Sajdah. Kisha utainuka na kutulia katika kikao kisha utafanya hivyo katika swalah zote.”

MAELEZO

Hii ni nguzo ya tisa miongoni mwa nguzo za swalah ambayo ni utulivu. Maneno yake:

“Utulivu katika vitendo vyote.”

Katika kusimama, Takbiyrat-ul-Ihraam, kusoma al-Faatihah, Rukuu´, kuinuka kutoka katika Rukuu´, kusujudu, kuinuka kutoka katika Sujuud, kukaa kati ya Sujuud mbili. Kwa msemo mwingine katika matendo yote ya swalah.

Maana ya kutulia ni kusubiri mpaka kila kiungo cha mwili kirudi mahali pake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 89
  • Imechapishwa: 24/06/2022