58. Dalili ya nguzo zote


Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا

“Enyi mloamini! Rukuuni na sujuduni.”[1]

Ni dalili kuthibitisha kwamba Rukuu´ na Sujuud ni nguzo mbili.

Maneno yake mtunzi:

”Vilevile… ”

Dalili juu ya kwamba kusujudu juu ya viungo saba ni nguzo ni Hadiyth kwamba amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nimeamrishwa kujusudu juu ya viungo saba.”

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimeamrishwa kujusudu juu ya viungo saba; juu ya paji la uso – na akaashiria kwa mkono wake juu ya pua yake – mikono miwili, magoti mawili, ncha za vidole na kutokukunja nguo na nywele.”[2]

[1] 22:77

[2] al-Bukhaariy (810) na Muslim (490).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 88
  • Imechapishwa: 24/06/2022