Upande mmoja wanazuoni wengi hii leo wanaona kuwa uso wa mwanamke ni uchi na hivyo haifai kuuacha wazi. Utafiti uliotangulia unatosha katika kuwaraddi. Upande wa pili lipo kundi lingine linaloona kwamba kufunika uso ni Bid´ah na kuchupa mipaka katika dini, kama yalivyotufikia hayo kutoka kwa baadhi ya ndugu wanaoshikamana na Sunnah huko Lebanon. Kwa ndugu hawa na wengine nawaandikia yafuatayo:

Mwanamke kufunika uso na mikono ni jambo lina msingi katika Sunnah. Mambo hayo yalikuwa yakifanywa katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama yanavyoashiria maneno yake:

”Haifai kwa mwanamke aliye katika Ihraam kujifunika kwa Niqaab na kuvaa vifuniko vya mikono.”[1]

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Haya yanafahamisha kuwa Niqaab na vifuniko vya mikono vilikuwa vinatumiwa na wanawake ambao hawako katika Ihraam, jambo ambalo linapelekea kufunika nyuso na mikono yao.”[2]

[1] al-Bukhaariy, an-Nasaa’iy, al-Bayhaqiy na Ahmad kupiita kwa Ibn ´Umar, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[2] Tafsiyr Suurat-in-Nuur, uk. 56

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 104
  • Imechapishwa: 03/10/2023