Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mwambie:

“Vipi utajitakasa nafsi yako na shirki na wewe huijui? Ni vipi Allaah atakuharamishia wewe jambo hili na kutaja ya kwamba hatolisamehe, wakati wewe huliulizii na wala hulijui? Wafikiria ya kwamba Allaah atatuharamishia na wala asitubainishie?”

MAELEZO

Akijitakasa nafsi yake na shirki kwa kuwaelekea watu wema, atajibiwa kwa njia mbili:

1 – Ni vipi utajitakasa nafsi yako na shirki ilihali huijui? Mtu atahukumu jambo vipi kabla ya kulielewa? Kuona kuwa nafsi yako imetakasika na shirki na wewe huitambui, ni kuhukumu pasi na elimu.

2 – Ni kwa nini huulizi juu ya shirki hii ambayo Allaah (Ta´ala) ameiharamisha na ambayo ni khatari zaidi kuliko mauaji na uzinzi na inamuwajibishia mwenye nayo Moto na Pepo ni haramu kwake? Unadhani ya kwamba Allaah amewaharamishia waja Wake pasi na kuwabainishia nayo? Kamwe!

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 25/11/2023