Imani inazidi kwa utiifu na inashuka kwa maasi. Amesema (Ta´ala):

فَزَادَهُمْ إِيمَانًا

“Yakawazidishia imani.”[1]

لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَّعَ إِيمَانِهِمْ

”Ili awazidishie imani pamoja na imani zao.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atatolewa ndani ya Moto yule aliyesema “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” na moyoni mwake mna imani kiasi cha punje ya ngano, mbegu ya haradali au vumbi nafaka.”[3]

al-Bukhaariy amepokea mfano wake.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafanya imani ni yenye kutofautiana. Kukithibiti kuzidi kwake ndio kumethibiti kushuka kwake. Kwa sababu chenye kuzidi ni lazima kabla ya hapo kiwe kimeshuka ndio kikazidi.

[1] 03:173

[2] 48:04

[3] al-Bukhaariy (44) na Muslim (193).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 99
  • Imechapishwa: 07/11/2022