Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

37 – Hakuna yeyote awezaye kurudisha nyuma mipango Yake, kupinga hukumu Yake wala kushinda amri Yake.

MAELEZO

إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ

“Anapotaka chochote hukiambia: “Kuwa!” nacho huwa.”[1]

وَاللَّـهُ يَحْكُمُ لَا مُعَقِّبَ لِحُكْمِهِ ۚ وَهُوَ سَرِيعُ الْحِسَابِ

“Allaah anahukumu na hakuna wa kupinga hukumu Yake; Naye ni Mwepesi wa kuhesabu.”[2]

Wakati Allaah (´Azza wa Jall) anapohukumu jambo lolote, basi hakuna yeyote awezaye kulipinga au kulirudisha nyuma. Hivyo ni tofauti na inavyokuwa kwa hukumu za viumbe ambazo zinaweza kupingwa na kutenguliwa. Hakuna yeyote awezaye kushinda amri Yake ya kilimwengu. Kuhusu amri Yake ya kidini inaweza kutenguliwa na kukhalifiwa. Hivo ndivo Allaah anavyowajaribu na kuwatahini viumbe ili apate kuwalipa thawabu au kuwaadhibu.

[1] 36:82

[2] 13:41

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 55
  • Imechapishwa: 07/11/2022