Jengine ni kwamba ´ibaadah hii imegawanyika katika ´ibaadah ya kimwili na ´ibaadah ya kimali.

´Ibaadah za kimwili ni zile aina tatu tulizotaja. ´Ibaadah hii inakuwa kupitia mdomo, viungo vya mwili na moyoni.

´Ibaadah za kimali. Kama mfano wa kutoa zakaah na mtu kujitolea katika njia ya Allaah ambayo ni jihaad. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ

“Wakazipinga kwa dhuluma na majivuno na hali kuwa nafsi zao. “[1]

Amezitanguliza mali juu ya nafsi. Kupambana jihaad kwa mali ni ´ibaadah ya kimali.

Hajj ndani yake kuna ´ibaadah ya kimwili na ´ibaadah ya kimali. Kutekeleza zile taratibu za hajj, Twawaaf, Sa´y, kurusha vijiwe kwenye viguzo, kusimama ´Arafah na kulala Muzdalifah ni ´ibaadah za kimwili. Ama kujitolea kwa ajili yake ni ´ibaadah ya kimali. Kwa sababu hajj inahitajia mtu kujitolea.

[1] 27:14

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 124
  • Imechapishwa: 23/12/2020