Mimi nimeeleza kwa kina nukuu hizi kutoka kwa Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab kuhusu kuthibitisha suala hili, nalo ni kuwa kumkufurisha mtu mmojammoja aliyeangukia katika shirki ya ´ibaadah kwa sababu ya ujinga wake kunatokea baada ya kubainishiwa na kusimamishiwa hoja, si kabla ya hapo. Kwa sababu miongoni mwa wajinga na wenye chuki dhidi yake na dhidi ya ulingano wake – uliyojengwa juu ya Qur-aan na Sunnah na juu ya yale yaliyokuwa juu yake Salaf wa ummah – wapo wanaompaka matope na kuwafanya watu wakimbie mbali na ulingano wake kwa kumtuhumu kwamba anakufurisha waislamu kwa ujumla na kwamba anakufurisha kwa jumla. Ilhali ukweli wa mambo ni kwamba yeye hakumkufurisha isipokuwa yule aliyesimamishiwa hoja na njia ikawa wazi kwake. Jengine ni kwa sababu baadhi ya wachache miongoni mwa wanafunzi katika Ahl-us-Sunnah – kama nilivyofahamu – wanamkosoa yule anayebainisha jambo hili. Kufanya hivo ni kukosoa kwa kile walichokibainisha Mashaykh wawili; Ibn Taymiyyah na Muhammad bin ‘Abdul-Wahhaab na wengineo miongoni mwa wanazuoni. Pamoja na hayo hakika kosa katika kusamehe katika mambo yenye mushkili ni bora kuliko kosa katika kutoa adhabu.
Isitoshe wao, kwa kuikosoa maoni yaliyothibitishwa na Mashaykh wawili na wakashikamana na kinyume chake, wanafungua njia kwa wale wanaovizia Ahl-us-Sunnah ambao huvua samaki katika maji machafu na hurudia matamshi ya maadui wa Uislamu na waislamu wanaodai kuwa msimamo mkali wa wale waliopatikana na vitendo vya kulipua na kuharibu unatokana na kujifunza mtaala wa elimu uliojengwa juu ya vitabu vya Shaykh Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab na wengineo miongoni mwa Ahl-us-Sunnah, jambo ambalo ni uzushi na uongo uliozuliwa na kuenezwa. Kwani wale walioyarudia maneno haya miongoni mwa watu wa nchi hii walijifunza kama walivyojifunza wengine mtaala huu na wala hawakupata madhara yoyote kutokana nao, bali walipata manufaa makubwa kutoka humo kila aliyependa Allaah amuongoze na ampe tawfiyq. Isipokuwa wale waliopindukia mipaka walitoka nje kwa sababu ya uelewa wao mbovu ambao walienda kinyume nacho na wakatoka katika umoja wa waislamu. Kigezo chao katika hilo ni Khawaarij waliotoka na kuwapinga Maswahabah kwa sababu ya uelewa wao potofu – na kila watu wana warithi wake. Allaah ndiye Mwenye kutakwa msaada.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 78-80
- Imechapishwa: 01/07/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 78-80
Imechapishwa: 01/07/2026
https://firqatunnajia.com/57-hapa-ndipo-anakufurishwa-mjinga-aliyeingia-katika-shirki/