56. Ni upi mfumo wa Ahl-us-Sunnah katika kuwakosoa watu na kuwataja majina yao?

Swali 56: Ni upi mfumo wa Ahl-us-Sunnah katika kuwakosoa watu na kuwataja majina yao? Je, ni uchokozi na imekatazwa kuyataja makosa ya baadhi ya walinganizi?

Jibu: Kosa linatakiwa kubainishwa. Ni lazima kubainisha kosa kutokana na usawa. Hata hivyo hakuna faida yoyote kushambulia utu wa watu. Bali ni jambo lenye madhara. Sisio watu wanaotuhusu. Hakika hapana vyenginevyo tunayabainisha makosa. Tunawabainishia pia watu haki ili waichukue haki na waacheni na makosa hayo. Malengo sio shakhsia za watu. Hilo si lengo. Ambaye lengo lake ni hayo yaliyotajwa huyo ni mtu anayefuata matamanio. Lakini yule ambaye lengo lake ni kuwabainishia watu haki huyo ndiye ambaye anawatakia waislamu mema.

Ikiwa kuna manufaa makubwa ya kumtaja yule mtu anayeraddiwa ili watu wamtambue ni sawa. Muhaddithuun huwataja kwa wale wasimulizi waliojeruhiwa na wakasema kwa mfano kuwa ni waongo, kumbukumbu dhaifu na mdanganyifu. Wanazibainisha hali zao. Malengo yao sio kumshambulia mtu yeye kama yeye. Malengo yao ni kuibainisha haki na ili msomaji ajue kuwa cheni ya wapokezi wake ina upungufu ili ajiepushe nayo. Kinachozingatiwa ni lile kusudio. Ikiwa kusudio ni yule mtu yeye kama yeye, basi hayo ni matamanio – na ni jambo halijuzu. Na ikiwa malengo ni kuibainisha haki na kuwatakia watu kheri, haina neno kufanya hivo[1].

[1] Ibn-ul-Mubaarak amesema:

”Mu´allaa bin Hilaal anasema uwongo wakati anapozisimulia Hadiyth.” Baadhi ya Suufiyyah wakasema: ”Ee Abu ´Abdir-Rahmaan! Unasengenya?” Akasema: ”Nyamaza! Tusipobainisha ni vipi itatambulika haki kutokana na batili?” (al-Kifaayah, uk. 9)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 155-156
  • Imechapishwa: 07/03/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy