Swali 55: Kubainisha makosa ya baadhi ya vitabu vya kivyamakivyama au makundi yaliyoingia nchini mwetu kunahesabika ni kuwatukana walinganizi?

Jibu: Hapana. Huku sio kuwatukana walinganizi[1]. Kwa sababu vitabu hivi sio vitabu vya ulinganizi. Watu wa vitabu na fikira hizi sio katika watu wanaolingania kwa Allaah kwa utambuzi, elimu na juu ya haki. Sisi pindi tunapobainisha makosa ya vitabu hivi, au makosa ya walinganizi hawa, hatufanyi hivo kwa lengo la kuwajeruhi watu wao kama wao. Tunafanya hivo kwa ajili ya kuutakia mema ummah[2] ili usifikwe na fikira zinazotia shaka. Baada ya hapo kukatokea mtihani na mipasuko. Lengo letu sio watu wenyewe. Lengo letu ni zile fikira zilizomo ndani ya vitabu hivyo ambavyo vimetuingilia kwa kutumia jina la ulinganizi.

[1] Walinganizi wa Salafiyyah hawazingatii kuwatahadharisha Ahl-ul-Bid´ah, wapotevu, mapote ya Hizbiyyah yaliyopo leo na vitabu vyao kuwa ni usengenyi. Bali wanaona kuwatahadharisha Ahl-ul-Bid´ah na vitabu vyao ni katika mfumo wa Salaf. Kuna mapokezi mengi mno yanayoshuhudia hilo. Bali wanamwabudu Allaah kwa matahadharisho hayo. Shu´bah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Njoo ili tusengenye kwa ajili ya Allaah kitambo fulani.” (Sharh ´Ilal at-Tirmidhiy (1/349) na al-Kifaayah (91))

Bi maana kujeruhi na kusifu.

Abu Zur´ah ad-Dimashqiy amesema:

”Nimemsikia Abu Mishar akiulizwa juu ya mtu ambaye anakosea katika masimulizi yake na anaandika makosa ambapo akajibu: ”Libainishe jambo lake.” Nikamwambia Abu Zur´ah: ”Huoni kuwa kufanya hivo ni usengenyi?” Akajibu: ”Hapana.” (Sharh ´Ilal at-Tirmidhiy (1/349))

´Abdullaah bin Imaam Ahmad amesema:

”Abu Twuraab an-Nakhshabiy alikuja kwa baba yangu ambapo baba yangu akasema kuwa fulani ni mnyonge na fulani ni mwenye kuaminika. Abu Twurab akasema: ”Ee Shaykh! Usiwasengenyi wanazuoni.” Ndipo baba yangu akamgeukia na kusema: ”Ole wako! Huku ni kuwatakia watu kheri, sio kusengenya.” (Sharh ´Ilal at-Tirmidhiy (1/349-350) na al-Kifaayah (46))

Hata hivyo walinganizi wenye kutia shaka ndio ambao huathirika wakati wanapokosolewa Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ (kama wako hai) na vitabu vyao na kutahadharishwa.

[2] Ijapo kufanya hivo ni kuwajeruhi wanamme katika uadilifu wao na kuwasifia. Yanafanywa hayo ili mtu asidanganyike nao, khaswakhaswa ikiwa mtu ana taathira na anao wafuasi kama wale viiongozi wa harakati mbalimbali. Haya yanapatikana katika vitabu vya kujeruhi na kusifia na vitabu vya wasifu. Hilo halina ubaya kwa ambaye upeo wa kufanya hivo. Lengo ni kutambulisha hali ya mtu na kutahadharisha naye na si yeye kama yeye. Pindi Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) alipoulizwa juu ya Husayn al-Karaabiysiy akasema:

”Ni mzushi.” (Taariykh Baghdaad (8/66))

Wakati alipoulizwa juu ya al-Muhaasibiy akasema:

”Usidanganyike na unyenyekevu na upole wake. Usidanganyike na kuinamisha kwake kichwa. Ni mtu muovu. Hakuna anayemtambua isipokuwa tu yule mwenye uzoefu naye! Usizungumze naye. Hatakiwi kuonyeshwa heshima. Je, wewe unakaa na kila mzushi anayesimulia Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Hapana. Hatakiwi kuonyeshwa heshima!”  (Twabaaqaat-ul-Hanaabilah (1/233))

Abu Zur´ah amesema wakati alipoulizwa juu ya al-Haarith al-Muhaasibiy na vitabu vyake:

”Usidanganyike na unyenyekevu na upole wake. Usidanganyike na kuinamisha kwake kichwa. Ni mtu muovu. Hakuna anayemtambua isipokuwa tu yule mwenye uzoefu naye! Usizungumze naye. Hatakiwi kuonyeshwa heshima. Je, wewe unakaa na kila mzushi anayesimulia Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Hapana. Hatakiwi kuonyeshwa heshima!”  (Twabaaqaat-ul-Hanaabilah (1/233))

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 146-147
  • Imechapishwa: 07/03/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy