56. Kuswali na kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni shirki

Hivyo mwambie: “Kwa hiyo unajua Kauli ya (Ta´ala):

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

”Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako.” (al-Kawthar 108 : 02)

ukamtii Allaah na ukamchinjia; je hii itazingatiwa kuwa ni ´Ibaadah?” Hana budi kusema: “Ndio”.

MAELEZO

Ukianza kumsomea Aayah na Hadiyth ya kwamba du´aa ni ´ibaadah ni lazima akubali. Halafu muulize endapo atamuomba Allaah usiku na mchana lakini baadhi ya nyakati akawa anamuomba asiyekuwa Allaah – je, atakuwa mshirikina? Ni lazima akubali na kusema kuwa ni mshirikina kwa kuwa amemuomba asiyekuwa Allaah na mwenye kumuomba asiyekuwa Allaah anakuwa mshirikina. Ikiwa yule anayemuomba asiyekuwa Allaah, ijapokuwa mara moja tu maishani, anakuwa mshirikina – pamoja na kuwa anamuomba Allaah usiku na mchana – vipi kuhusu wale wenye kuwaomba na kuwataka kinga daima wengine na kusema “Ee al-Husayn! Ee Badawiy! Ee ´Abdul-Qaadir! Ee fulani na fulani!”. Watu kama hawa wanafanya shirki sana. Ikiwa yule mwenye kumchinjia asiyekuwa Allaah au akaswali kwa ajili ya asiyekuwa Allaah anakuwa mshirikina, vipi kwa yule anayemuomba kinga asiyekuwa Allaah katika kutatua matatizo – je, mtu kama huyu hawi mshirikina? Jibu ni ndio. Kwa kuwa mlango ni mmoja. Aina za ´ibaadah zote mlango wake ni mmoja. Haijuzu kumtakasia ´ibaadah katika baadhi yake na kumshirikisha Allaah katika baadhi ya zengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 84
  • Imechapishwa: 13/01/2017