Ni ipi hukumu ya swalah ya mwendawazimu?

Swali: Kuna mwendawazimu ambaye hata hivyo anaswali baadhi ya nyakati katika hali ya wendawazimu wake. Je, anapewa thawabu kwa swalah yake?

Jibu: Ikiwa ana fahamu ndani yake anapewa thawabu kwayo. Ikiwa hana fahamu ndani ya swalah na wala haitambui inahesabika ni harakati anazofanya zisizokuwa na nia na malengo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2053
  • Imechapishwa: 13/01/2017