Swali: I´tikaaf ni kitu gani na ni zipi sharti zake?

Jibu: I´tikaaf ni kule kulazimiana na kubaki msikitini kwa lengo la kumtii Allaah. Sharti zake mtu abaki na awe msikitini. Asitoke isipokuwa kutokana na haja ambayo hakuna mwengine awezaye kuifanya isipokuwa yeye tu, kama vile kula, kunywa na kukidhi haja.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 45
  • Imechapishwa: 02/04/2022