Swali: Ni majuzu mangapi ya Qur-aan mtu anaweza kusoma siku ya Ramadhaan?

Jibu: Soma kiasi unachoweza, lakini kwa kuzingatia na kuelewa maana. Kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kusoma Qur-aan basi anapata kwa kila herufi mema kumi. Sisemi kuwa Alif, Laam na Miym ni herufi moja. Lakini Alif ni herufi moja, Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja.”[1]

[1] at-Tirmidhiy na al-Haakim kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Kadhalika ameipokea al-Aajurriy katika ”Aadaab Hamalat-il-Qur-aan”. Imetajwa katika ”as-Swahiyhah” (569).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 45
  • Imechapishwa: 02/04/2022