55. Nguzo ya sita: Kunyooka sawasawa


Maneno yake:

“… kunyooka sawasawa.”

Nguzo ya sita miongoni mwa nguzo za swalah ni kunyooka sawasawa. Anapomaliza kurukuu na akainua kichwa chake basi atatakiwa kunyooka sawasawa mpaka mpaka kila kiungo cha mwili kitue pahali pake. Dalili ya nguzo mbili hizi – nguzo ya tano na ya sita – ni yale yaliyoko katika ile Hadiyth ya yule bwana aliyeswali vibaya – itakuja katika maneno ya mtunzi wa kitabu:

“Unapoenda katika Rukuu´ basi weka vitanga vyako vya mikono juu ya magoti yako, unyooshe mgongo wako na tulizana kwenye Rukuu´ yako.“

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 87-88
  • Imechapishwa: 23/06/2022