56. Nguzo ya sita: Kusujudu juu ya viungo saba

Maneno yake:

“… kusujudu juu ya viungo saba.”

Nguzo ya saba miongoni mwa nguzo za swalah ni kusujudu juu ya viungo saba. Viungo saba, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh), ni mikono miwili, magoti mawili, ncha za vidole, paji la uso na pua – navyo vinazingatiwa ni kiungo kimoja.

Akinyanyua kiungo kimoja miongoni mwa viungo hivi saba kuaniza mwanzoni mwa kusujudu kwake mpaka mwishoni mwake basi Sujuud haisihi. Endapo atanyanyua kiungo kimoja miongoni mwa viungo hivyo kisha akakirudisha Sujuud itasihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 88
  • Imechapishwa: 23/06/2022