55. Mfungaji anatakiwa kujiepusha na kusema uongo

Miongoni mwa adabu za lazima ni mfungaji kujiepusha na yale yote aliyoharamisha Allaah na Mtume Wake katika maneno na vitendo. Hivyo ajiepushe na uongo. Nako ni kule kueleza kinyume na uhalisia wa mambo. Kubwa zaidi ni kule kumsemea uongo Allaah na Mtume Wake. Kama kumwegemezea Allaah au Mtume Wake uhalalishaji wa haramu au uharamishaji wa halali. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ مَتَاعٌ قَلِيلٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Na wala msiseme zinazosifia ndimi zenu uongo: hii halali na hii haramu ili mumzulie Allaah uongo. Hakika wale wanaomzulia Allaah uongo hawafaulu. Ni starehe ndogo tu na watapata adhabu iumizayo.”[1]

al-Bukhaariy, Muslim na wengineo wamepokea kupitia kwa Abu Hurayrah na wengineo kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kunisemea uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake Motoni.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametahadharisha uongo na akasema:

“Tahadharini na uongo. Kwani hakika uongo unaelekeza katika uovu na hakika uovu unaelekeza kwenda Motoni. Hatoacha mtu kusema uongo na kuupa kipaumbele uongo mpaka aandikwe mbele ya Allaah kuwa ni mwongo.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] 16:116-117

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 69-70f
  • Imechapishwa: 20/04/2021