8 – Abu Mansuur Ma’mar bin Ahmad amesema:

“Nilipouona ugeni wa Sunnah, wingi wa Bid´ah na kufuata matamanio, ndipo nikataka kutumia fursa ya kuwausia marafiki zangu na waislamu waliosalia nyasia za ´Aqiydah na mawaidha yenye hekima, na yale waliyoafikiana kwayo Ahl-ul-Hadiyth wal-Athar, watambuzi na masufi, katika wema waliotangulia na wengineo waliokuja nyuma… na kwamba Allaah (´Azza wa Jall) amelingana juu ya ´Arshi Yake, bila ya kuifanyia namna, kuifananisha wala kuipindisha maana. Kulingana juu kunatambulika na namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini jambo hilo na ni ukafiri kupinga jambo hilo. Yeye (´Azza wa Jall) amelingana juu ya ´Arshi Yake – pasi na kumfanyia namna. Na kwamba Yeye (´Azza wa Jall) ametengana mbali na viumbe Wake kama ambavo viumbe pia wametengana Naye mbali. Hakuna maingiliano, mchanganyiko wala kuambatana. Kwa sababu Yeye ni Mmoja na aliyejitenga mbali na viumbe Wake. Ujuzi Wake umeenea kila mahali na hakuna popote inapokosekana ujuzi Wake.”[1]

9 – Ibn Qutaybah amesema:

“Inapokuja katika masimulizi haya, sahini ni kuamini yale yote yaliyosihi kupitia nukuu za wasimulizi madhubuti. Tunaamini Kuonekana na Kujidhihirisha na kwamba Yeye anastaajabishwa, anashuka katika mbingu ya chini kabisa ya dunia, amelingana juu ya ´Arshi na kwamba yuko na Nafsi na mikono miwili. Haitakiwi kwetu kumfanyia namna, kikomo wala kumlinganisha na chochote kile. Tunataraji kwa ´Aqiydah hiyo kesho tutakuwa katika njia okovu – Allaah akitaka.”[2]

Maneno yenye manaa kama hiyo kutoka kwa Salaf ni mengi. Miongoni mwao, ingawa sikupata cheni yake ya wapokezi, ni jawabu la Ash-Shaafiy’iy wakati alipoulizwa kuhusu Kulingana juu:

”Naamini bila ya kushabihisha na nasadikisha bila ya kufananisha. Naituhumu nafsi yangu kudiriki na najiepusha hali ya juu kupekua.”[3]

Inasemekana kwamba Ahmad amesema:

”Amelingana juu kama Alivyotaja, na sio kama anavyofikiria mtu.”[4]

Na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kama alivosema mshairi:

Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi Yake,

kama vile ilivyoeleza Qur-aan na Mteule

Kulingana juu huko kunaendana na utukufu Wake

na najitenga mbali na yule mwenye kusema kuwa ametawala ´Arshi

Yeye anayesema kwamba kulingana Kwake juu ni kama kupanda safina

ya mlima al-Juudiy amejitupa ndani ya shimo

Yule anayefuata yale yasiyokuwa wazi

kwa sababu ya kutaka fitina au tafsiri mbovu ni mpotevu

Sisemi kuwa ametawala wala

sina jukumu la kufasiri – kamwe!

Na yule anayeniuliza Amelingana namna gani

hakuna nitamchomjibu zaiid ya kumwambia: Amelingana juu![5]

[1] al-Hujjah fiy Bayaan-il-Mahajjah (1/232).

[2] al-Ikhtilaaf fiyl-Lafdhw war-Radd ´alaal-Jahmiyyah wal-Mushabbihah, uk. 53.

[3] Aqaawiyl-uth-Thiqaat, uk. 121, ya al-Karmiy.

[4] Aqaawiyl-uth-Thiqaat, uk. 121, ya al-Karmiy.

[5] Tazama “al-Kawaakib ad-Durriyyah”, uk. 28, ya Ibn Maaniy´.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 15/12/2025