Kuna mapote mawili yaliyoenda kinyume katika mipango na makadirio:
1 – Jabriyyah. Wanasema kuwa mja ametenzwa nguvu juu ya matendo yake na hana khiyari katika jambo hilo. Tunawaraddi kwa mambo mawili:
1 – Allaah ameyaegemeza matendo ya mtu kwake na amefanya kuwa yeye ndiye ameyachuma; anaadhibiwa na analipwa thawabu kutokana na vile atakavyotenda. Angekuwa ametenzwa nguvu basi isingesihi kumnasibishia nayo na kule kumuadhibu kwayo ingelikuwa ni dhuluma.
2 – Kila mmoja anajua tofauti kati ya kitendo ambacho mtu anakifanya kwa kutaka kwake mwenyewe na asichofanya kwa kutaka kwake inapokuja katika ule uhakika na hukumu. Endapo mtu atamshambulia mwingine na akadai kuwa ametenzwa nguvu juu ya kufanya hivo kutokana na mipango na makadirio ya Allaah, basi kitendo hicho kingezingatiwa kuwa ni upumbavu unaoenda kinyume na yanayotambulika kilazima.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 96
- Imechapishwa: 06/11/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)