53. Mfumo uleule, vyombo vingine

Shaykh Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mifumo na njia za ulinganizi hii leo na kabla yake na baada yake ni lazimauwe ule mfumo wa ulinganizi ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumilizwa nao na akatimiza kwazo lengo lake. Kitu kinachoenda kinyume hii leo, ni kwa mfano pambanuzi zinazofungamana na misingi yake ndani ya Qur-aan na Sunnah. Mfano wa pambanuzi hizo ni mashirika ya vyombo vya mawasiliano – ambavyo vinakubaliwa na Shari´ah, ambavyo hii leo vinafanya mfumo wa ulinganizi. Kuanzia mwanzoni mwa Uislamu njia hii ilijenga ulinganizi, kwa sababu kipindi hicho ulinganizi ulikuwa unategemea neno. Mashirika ya vyombo vya mawasiliano vimebaki ni vilevile, lakini muda ulivyokuwa unaenda vikafanywa upya. Ikiwa ulinganizi ulifanywa kwa neno, basi mambo ni vivyo hivyo ikiwa neno litasikiwa, litasomwa na kadhalika.

Mfano mwingine ni mashirika ya elimu na shule za kinidhamu. Mambo haya hayakutofautiana na ule mfumo uliojenga Uislamu kuanzia mwanzo wa Uislamu. Ikiwa ulinganizi unategemea mafunzo; Hadiyth ya Jibriyl (´alayhis-Salaam) inayotambulika kuhusu Uislamu, imani na ihsaan ni mfano mzuri wa ulinganizi kwa njia ya kufundisha. Kwa hivyo njia ya kufunza ya leo ndio ileile iliokuwa hapo jana, lakini muda ulivyokuwa unaenda ikafanywa upya. Lakini mabadiliko haya ni lazima yawe ndani ya mzani wa Qur-aan na Sunnah. Wakati kunapozuka kasoro katika mabadiliko hayo, basi ni lazima kukiweka mbali na kukitenga mbali nayo. Mfumo mpya unaozuka kamwe hautakiwi kufanywa ni kitu cha kuabudia kwacho.”[1]

Kwa haya inapata kubainika ya kwamba vyombo hivi vya kisasa na maendeleo ya ustaarabu hayagongani kabisa na ulazima wa kwamba ulinganizi ni lazima uwe kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah kwa sharti vyombo hivi vya kisasa na maendeleo ya ustaarabu yaafikiane na mzani wa Qur-aan na Sunnah; kile kinachokubaliwa na Shari´ah, basi kitatumika kwa jina na ulinganizi, na kile kinachokataliwa na Shari´ah, kitarudishwa nyuma na hakitotumiwa. Yale ambayo Allaah (Ta´ala) ameyaruhusu yanatosheleza kutokamana na yale aliyoyaharamisha na kuyatakaza. Yale ambayo Allaah (Ta´ala) ametuwekea katika Shari´ah na akatusahilishia kwa dini Yake nyepesi na ya kupwekesha kupitia kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), yanawatoshakutokamana na Ummah kuhitajia kila batili, haramu na chenye kudhuru[2].

[1] Hukm-ul-Intimaa’, uk. 160-161

[2] Tazama ”Ighaathat-ul-Lahfaan” (2/69).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 28/05/2023