Miongoni mwa mambo yatayokuwa siku ya Qiyaamah ni hesabu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) atawafanyia hesabu viumbe siku ya Qiyaamah. Kafiri atafanyiwa hesabu ya kuthibitishiwa na sio hesabu kwa njia ya kupimiwa kati ya mema na maovu. Kwa sababu kafiri hana mema yoyote. Atathibitishiwa matendo yake ya ukafiri.
Ama waumini watafanyiwa hesabu juu ya matendo yao. Kwa sababu wao wana matendo mema na maovu. Lakini wako pia ambao hawatafanyiwa hesabu na wataingia Peponi bila ya hesabu, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth ya wale watu elfu sabini wataoingia Peponi bila hesabu wala adhabu[1]. Miongoni mwao wako ambao watafanyiwa hesabu nyepesi ambayo ni kule kuonyeshwa:
فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا
“Atahesabiwa hesabu nyepesi na atageuka kwa ahli zake hali ya kuwa ni mwenye kufurahi.”[2]
Wako wengine ambao watajadiliwa katika hesabu. Watafanyiwa hesabu ya majadilio[3].
[1] al-Bukhaariy (6541) na Muslim (220) kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).
[2] 84:08-09
[3] Tazama ”Swahiyh-ul-Bukhaariy” (103) na ”Swahiyh-ul-Muslim” (2876).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 78-79
- Imechapishwa: 07/04/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)