Amesema (Rahimahu Allaah):

“Naamini kuwa Njia itawekwa juu ya ukingo wa Jahannam na watu watapita juu yake kutegemea matendo yao.”

Baada ya hali zote hizi ipo Njia iliyowekwa katikati ya Jahannam. Viumbe wote watapita juu ya Njia hii. Ni nyembamba kuliko unywele, yenye makali zaidi kuliko upanga na yenye kuunguza zaidi kuliko kaa la moto. Watu watapita juu yake kutegemea matendo yao. Matendo yao ndio yatawapitisha juu ya njia.

Miongoni mwao wako ambao watapita kama umeme.

Miongoni mwao wako ambao watapita kama farasi aendae mbio.

Miongoni mwao wako ambao watapita kama mpanda ngamia.

Miongoni mwao wako ambao watapita kwa kukimbia.

Miongoni mwao wako ambao watapita kwa kutembea.

Miongoni mwao wako ambao watapita kwa kutambaa.

Miongoni mwao wako ambao watakamatwa na kutupwa ndani ya Moto.

Haya yametajwa ndani ya Qur-aan. Amesema (Ta´ala):

فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَـٰنِ عِتِيًّا ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا

”Naapa kwa Mola wako, bila shaka Tutawakusanya wao na mashaytwaan, kisha tutawahudhurisha pembezoni mwa Moto hali ya kupiga magoti, kisha bila shaka tutawachomoa katika kila kundi wale ambao waliomuasi zaidi Mwingi wa rehema, kisha bila shaka Sisi tunawajua zaidi wale wanaostahiki zaidi kuchomwa humo. Na hakuna yeyote miongoni mwenu isipokuwa ataufikia.”[1]

Kila mtu atapita juu ya Moto:

وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا

“Na hakuna yeyote miongoni mwenu isipokuwa ataufikia. Hiyo kwa Mola wako ni hukumu ya lazima kutimizwa. Kisha tutawaokoa wale waliomcha Allaah na tutawaacha madhalimu humo wamepiga magoti.”[2]

Wakivuka njia watasimamishwa kwa ajili ya kulipiza kisasi. Watalipizana kisasi kati yao. Wakishasafika ndio watapewa idhini ya kuingia Peponi.

[1] 19:68-71

[2] 19:71-72

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 79-81
  • Imechapishwa: 07/04/2021