52. ´Aqiydah ya Ibn ´Abdil-Wahhaab juu hodi, hesabu na njia


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Naamini Hodhi ya Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika uwanja wa Qiyaamah. Maji yake ni meupe mno kuliko maziwa na matamu zaidi kuliko asali. Vikombe vyake ni sawa na idadi ya nyota mbinguni. Mwenye kunywa kutoka humo mara moja basi kamwe hatohisi kiu tena baada yake.

Naamini kuwa Njia itawekwa juu ya ukingo wa Jahannam na watu watapita juu yake kutegemea matendo yao.

MAELEZO

Miongoni mwa mambo yatayokuwa siku ya Qiyaamah ni Hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni Hodhi ambayo urefu wake ni mwendo wa mwezi mmoja na upana wake ni mwendo wa mwezi mmoja. Maji yake ni meupe mno kuliko maziwa na matamu zaidi kuliko asali. Vikombe vyake ni sawa na idadi ya nyota mbinguni. Mwenye kunywa kutoka humo mara moja basi kamwe hatohisi kiu tena baada yake[1]. Ummah wake wataiendea na yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) awape maji. Wako watu ambao watataka kwenda wazuiwe. Aseme: “Ee Mola! Maswahabah zangu.” Aambiwe: “Wewe hujui kile walichozua bada yako.”[2]

Watazuiwa kuiendea Hodhi. Hao ni wale ambao walileta na kuzusha mambo mepya katika dini. Watazuiwa kuifikia Hodhi. Maneno yake:

“… katika uwanja wa Qiyaamah.”

Ni sehemu pana.

[1] Tazama ”Swahiyh-ul-Bukhaariy” (6579) na ”Swahiyh-ul-Muslim” (2292).

[2] al-Bukhaariy (6576) na Muslim (2297) kupitia kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 78
  • Imechapishwa: 07/04/2021