52. Wudhuu´ wa Mtume na ar-Rubayyi´ bint Mu´awwidh

10 – ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Aqiyl amesema:

 ” ´Aliy bin al-Husayn alinituma kwa ar-Rubayyi´ bint Mu´awwidh kumuuliza juu ya wudhuu´ wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu alikuwa akitawadha kwake. Nilipomwendea akachukua chombo na kusema: ”Nilikuwa nikifanya namna hii pindi ninapomletea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maji kwa ajili ya kutawadha.”[1]

[1] al-Humaydiy katika “al-Musnad”, at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” na wengineo. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri licha ya makinzano yaliyopo juu ya ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Aqiyl, kama alivosema Ibn-ul-Qattwaan.

Nimetaja upokezi mfano wake katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” na humo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia mwanamke huyo:

”Nimiminie maji.”

Kwa at-Twabaraaniy imekuja:

”Nimiminie maji juu yangu.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

”Nilikuwa nikimimina maji kwenye mikono yake mara tatu.”

Kwa maana hiyo inaweza kutajwa katika kipengele cha kabla yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 101
  • Imechapishwa: 27/09/2023