156-
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُمْ وَارْحَمْهُمْ، وَعَافِهِمْ وَاعْفُ عَنْهُمْ، وَأَكْرِمْ نُزُلَهُمْ، وَوَسِّعْ مُدْخَلَهُمْ، وَاغْسِلْهُمْ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ، وَنَقِّهِمْ مِنْ الْخَطَايَا كَمَا نَقَّيْتَ الثَّوْبَ الأَبْيَضَ مِنْ الدَّنَسِ، وَأَبْدِلْهُمْ دَارًا خَيْرًا مِنْ دَارِهِمْ، وَأَهْلاً خَيْرًا مِنْ أَهْلِهِمْ، وَزَوْجًا خَيْرًا مِنْ زَوْجِهِمْ، وَأَدْخِلْهُمْ الْجَنَّةَ، وَأَعِذْهُمْ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ[ وَعَذَابِ النَّارِ]
“Eee Allaah! Mghufurie na mrehemu, muafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake [kaburini] na mpanulie maingilio yake na muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama Ulivyoitakasa nguo nyeupe kutokamana na uchafu, mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake, jamaa bora kuliko jamaa zake, mke bora kuliko mke wake na mwingize Pepo na mlinde na adhabu ya kaburi na adhabu ya Moto.”[1]
157-
اللهُـمِّ اغْفِـرْ لِحَيِّـنا وَمَيِّتِـنا وَشـاهِدِنا، وَغائِبِـنا، وَصَغيـرِنا وَكَبيـرِنا، وَذَكَـرِنا وَأُنْثـانا. اللهُـمِّ مَنْ أَحْيَيْـتَهُ مِنّا فَأَحْيِـهِ عَلى الإِسْلام، وَمَنْ تَوَفَّـيْتَهُ مِنّا فَتَوَفَّـهُ عَلى الإِيـمان، اللهُـمِّ لا تَحْـرِمْنـا أَجْـرَهُ، وَلا تُضِـلَّنا بَعْـدَهُ
“Ee Allaah! Msamehe aliyehai katika sisi na aliyekufa katika sisi, aliyepo na asiyekuwepo, wadogo wetu na wakubwa wetu, wakiume wetu na wakike wetu. Ee Allaah! Ambaye utampa uhai katika sisi basi mpe uhai katika Uislamu na utayemfisha katika sisi basi mfishe juu ya imani. Ee Allaah! Usitunyime ujira Wake na wala usitupoteze baada ya yeye kuondoka.”[2]
158-
اللهم إن فلان ابن فلان في ذمتك وحبل جوارك، فقه فتنة القبر، وعذاب النار، وأنت أهل الوفاء والحق، فاغفر له وارحمه، إنك الغفور الرحيم
“Ee Allaah! Hakika fulani mwana wa fulani yuko katika dhimma Yako na kamba ya ujirani Wako, hivyo basi mlinde na fitina ya kaburi na adhabu ya Moto – Wewe ndiye mtekelezaji na wa haki, basi msamehe na mrehemu, kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[3]
159-
اللهم عبدك وابن أمتك احتاج إلى رحمتك، وأنت غني عن عذابه، إن كان محسنا فزد في حسناته، إن كان مسيئا فتجاوز عنه
“Ee Allaah! Mja Wako na mtoto wa kijakazi Wako ni muhitaji wa huruma Yako Nawe ni mkwasi wa kumuadhibu. Kwa hivyo akiwa ni mwema basi mzidishie katika mema yake na akiwa ni muovu msamehe.”[4]
[1] Muslim (02/663).
[2] Abu Daawuud (320), at-Tirmidhiy (1024), an-Nasaa´iy (1988), Ibn Maajah (01/480) na Ahmad (02/368). Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah (01/251).
[3] Ibn Maajah. Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah” (01/251). Pia ameipokea Abu Daawuud (03/211).
[4] al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye (01/359). Tazama ”Ahkaam-ul-Janaaiz”, uk. 125 ya al-Albaaniy.
- Muhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huswn-ul-Muslim
- Imechapishwa: 01/05/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
79. Du´aa ya kwanza ya kumuombea maiti
81- Aombe ndani yake zile du´aa zilizothibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika hizo nimesimamia nne: 1- ´Awf bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia maiti ambapo nikahifadhi kutoka katika du´aa yake akisema: اللهم اغفر له وارحمه، وعافه واعف عنه،…
In "13. Mlango wa kumi na tatu: Mlango wa kumi na tatu: Kuhusu kumswalia mtoto na aliyekufa shahidi"
44. Namna ya kukamilisha swalah ya jeneza kwa aliyejiunga amechelewa
Swali 44: Mswaliji anatakiwa kulipa swalah ya jeneza akiingia akakuta amekwishapitwa na baadhi ya sehemu yake[1]? Jibu: Atailipa papo hapo. Akijiunga na imamu katika Takbiyr ya tatu basi ataleta Takbiyr na kusoma al-Faatihah. Pindi imamu atapoleta Takbiyr ya nne basi naye ataleta Takbiyr ya pili kwa nisba yake na atamswalia…
In "Ahkaam-ul-Janaa-iz - Ibn Baaz"
Maiti wa kike anaombewa du´aa ya kupewa mume bora kama ilivyo kwa mwanamme?
Swali: Ikiwa jeneza ni la mwanamke wakati wa kumuombea du´aa mtu asome: اللهم أبدلها زوجًا خيرًا من زوجها “Ee Allaah! Mbadilishie mume bora kuliko mume wake.” au du´aa hii ni yenye kukomeka kwa mwanamme peke yake? Jibu: Anaweza kuombewa zile du´aa zilizopokelewa kwa njia iliyoenea: “Ee Allaah! Mfanyie atayoyakuta Kwako…
In "al-Luhaydaan kuhusu mazishi"