2 – Ismaa’iyl bin ‘Aliy al-Ayliy amesimulia kwamba amemsikia Sahl bin ´Abdillaah akisema huko Baswrah mwaka 280:
“Akili pekee haiwezi kumthibisha wa Milele na Asiyekuwa na mwisho juu ya ´Arshi. Haki imeisimamisha kwa lengo la kutoa dalili na elimu, ili nyoyo zipate mwongozo wa njia ya kumfikia na isiivuke. Hakuifaradhishia moiyo ujuzi wa vyanzo vyake, na kwa ajili hiyo uwepo Wake juu yake hautakiwi kufanyiwa namna. Haijuzu kuuliza amelingana vipi inapokuja kwa Yule ambaye ameumba kulingana juu. Hakuna kingine kinachompasa muumini isipokuwa kuridhia na kujisalimisha na yale yaliyosemwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwamba Yuko juu ya ´Arshi Yake… zandiki (الزنديق) ameitwa hivo kwa sababu ameyapima maneno mazito (وزن دق الكلام) kutokana na akili yake ya kichaa na kipimo chake cha matamanio, akaachana na masimulizi na kufuata kumwongozo wa Sunnah na kuifasiri Qur-aan kwa mujibu wa matamanio yake. Kutakasika ni kwa Yule ambaye mawazo hayawezi kumfanyia namna.”[1]
3 – Abu Haniyfah amesema katika “al-Fiqh al-Akbar”:
“Yale aliyotaja Allaah (Ta’ala) ndani ya Qur-aan kama vile Uso, Mkono na Nafsi, ni sifa Zake ambazo hazitakiwi kufanyiwa namna. Wala haitakiwi kusema kwamba mkono Wake maana yake ni uwezo au neema Yake, kwa sababu kufanya hivo kunakanusha sifa Zake. Hiyo ni ´Aqiydah ya Qadariyyah na Mu´tazilah. Mkono Wake ni sifa Yake isiyotakiwa kufanyiwa namna, na ghadhabu Yake na radhi Zake ni sifa Zake zisizotakiwa kufanyiwa namna.”[2]
4 – al-Athram amesimulia katika “Kitaab-us-Sunnah”: Ibraahiym bin al-Haarith al-‘Abbaadiy ametuhadithia: al-Layth bin Yahyaa ametuhadithia: Nimemsikia Ibraahiym bin al-Ash´ath akisema: Abu Bakr, rafiki yake al-Fudhwayl, akisema: Nimemsikia al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw akisema:
”Haitakiwi kwetu kufikiria sana Allaah yuko namna gani. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amejieleza Mwenyewe kwa njia ya wazi kabisa kwa kusema:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala haiwi awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.”[3]
Hakuna sifa iliyo wazi zaidi kuliko vile Alivyojieleza Mwenyewe. Sifa zote, kama vile Kushuka, Kucheka, Kujifakhari na Kutazama, zinatokea vile atakavyo; Anashuka atakavyo, anajifakhari atakavyo, Anacheka atakavyo, Anatazama atakavyo. Kwa hivyo haitakiwi kwetu kufikiria ni vipi yanatokea mambo hayo. Basi Jahmiy akikwambia kuwa anamkufuru Mola ambaye anashuka kutoka mahali Pake, wewe mwambie kuwa unamwamini Mola ambaye anafanya vile Atakavyo.”[4]
[1] Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (13/331-332). adh-Dhahabiy ameitaja katika ´Uluww kwa tamko lisemalo:
“Kwa sababu haijuzu kwa muumini kuulizia ni namna gani kulingana Kwake juu inapokuja kwa Yule ambaye ameumba kulingana juu.”
[2] Sharh al-Fiqh al-Akbar, uk. 36-37, ya ´Aliy al-Qaariy.
[3] 112:1-4
[4] Ibn Taymiyyah ameitaja katika “Dar’-ut-Ta´aarudhw” (2/23-24) na Ibn-ul-Qayyim katika “Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 105-106.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 74-75
- Imechapishwa: 15/12/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 74-75
Imechapishwa: 15/12/2025
https://firqatunnajia.com/52-anayafanya-kama-anavyotaka/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket